Ajira Tanzania, Kazi

Ajira Tanzania, Kazi Tanzania.

Jinsi ya kutafuta kazi au kujiajiri mwenyewe.

Kuongezeka kwa vyuo vikuu, na vyuo vya ufundi Tanzania kumeongeza kiu ya ajira Tanzania.
Tanzania ina uhaba wa ajira Tanzania, hii ni kwa sababu vijana wa Tanzania wanamaliza vyuo bila kuwa na mafunzo jinsi ya kujiajiri. Hata kama kuna wachache wanaotaka kujiajiri, mikopo Katika taasisi zetu za fedha hasa mabenki ni mgumu sana. Masharti ya kupata mkopo Katika mabenki yetu ni magumu sana.

Ajira serikalini nazo ni ngumu, ni adimu sana. Serikali inatakiwa itekeleze mipango yake kikamilifu hasa ule wa mkukuta na mkurabita. Vijana waliomaliza form four, form six na vyuo wawezeshwe ili waanzishe biashara. Vijana ni taifa la leo, vijana wanatakiwa wajiajiri na waajiri wenzao ili ajira ziongezeke. Kwa namna hii nguvu kazi ya taifa itatumika na uchumi wa taifa utakua. Millenium Development Goals haitatekelezeka kama tutaacha vijana wakae mitaani bila ajira. Uchumi wa Tanzania unaporomoka kwa sababu hakuna uzalishaji, njaa inakabili sehemu nyingi za nchi.


Kuna mashamba mengi ya kilimo au ufugaji yamekaa bure bila kuendelezwa. Kwa nini tusubiri wawekezaji wa nje ya nchi wakati hawa vijana wa Tanzania wanaweza kuendeleza haya mashamba?
Hata wawekezaji wa nje ya nchi wakija, watawatumia baadhi ya vijana kwa ujira mdogo, mshahara mdogo na faida yote itapelekwa nje ya nchi.Uchumi wa nchi utazidi kudidimia kama tuta waacha vijana wa Tanzania bila ajira.

Haya mashamba makubwa tuyagawa kwa vijana au watanzania wanaotaka kufanya kilimo ili kuondokana na tatizo la ajira Tanzania.